Tawahudi

Kuhusu ugonjwa wa mifupa unaoweza kuitwa kwa jina hili angalia usonji Usonji (pia tawahudi, kwa Kiingereza autism) ni tatizo la kinafsi na la kihisia linalowatokea watu tangu utotoni na kuathiri uwezo wao wa kuwasiliana na wengine. Wenye tatizo hilo hawaonekani watu wa kawaida. Muda mwingine hawapendi kuangalia wengine pale wanapozungumza nao, au hawapendi kushirikiana na watu wengine katika mambo kadhaa. Pia, hawako vizuri katika mawasiliano. Muda mwingine huwa hawawezi kuongea au kuzungumza na watu wengine. Mwishoni, hujijibu wenyewe. Wanaweza wakawa na shauku na kitu ambacho mtu mwingine (ambaye hana tatizo la usonji) hafikirii kina umuhimu. Mtu mwenye tatizo hilo anaelekea mara nyingi kurudiarudia matendo kadhaa, na anaweza kuhofia vitu katika mazingira yake yasiyoeleweka kama tatizo na wengine. Usonji ni ugonjwa wa ukuaji wa neva unaojumuisha kudhoofishwa kwa uwezo wa mwingiliano wa kijamii na mawasiliano, na kwa tabia finyu na ya kujirudiarudia. Dalili hizo huanza kabla ya mtoto kutimiza miaka mitatu. Ugonjwa wa akili kwa watoto huathiri uchakataji wa habari katika ubongo kwa kubadili jinsi seli za neva na sinepsi zake zinavyounganika na kujipanga; jinsi gani hilo hutokea haileleweki vizuri. Ni moja ya matatizo matatu yanayotambulika katika wigo wa ugonjwa wa akili wa watoto (ASDs), nyingine mbili zikiwa maradhi ya Aspaja, ambayo haicheleweshi ukuaji wa kiutambuzi na lugha, na Tatizo la Ukuaji Ulioenea-Usiofafanulika Vinginevyo (PDD-NOS), ambao hutambuliwa kikamilifu wakati vigezo vyote vya kawaida au Aspaja havijatimizwa. Usonji una msingi kamili katika jeni, ingawa mpangilio wa jeni za ugonjwa wa akili kwa watoto ni changamano na si bayana kama ASD inaelezeka zaidi kwa mabadiliko makuu ya jeni yasiyo ya kawaida, au kwa mchanganyiko usio wa kawaida wa aina tofauti za jeni ya kawaida. Katika matukio ya nadra, usonji unahusishwa sana na visababishi vya kasoro za kuzaliwa. Ubishi unakumba mapendekezo mengine ya visababishi vya kimazingira, kama vile metali nzito, viuawadudu au chanjo za utotoni; nadharia tete ya chanjo haiwezekani kibiolojia na inakosa ushahidi yakinifu wa kisayansi. Uenezi wa usonji ni karibu 1-2 kati ya watu 1,000, wakati uenezi wa ASD ni takriban matukio 6 kwa 1,000, huku idadi ya wanaume ikiwa mara nne kuliko ya wanawake. Idadi ya walioaguliwa kuwa na usonji umeongezeka kwa kasi tangu miaka ya 1980, kwa kiwango kutokana na mabadiliko katika jinsi ya uaguaji, swali la kama maambukizi shadidi yameongezeka halijafumbuliwa. Wazazi kwa kawaida hugundua dalili katika miaka miwili ya kwanza ya maisha ya mtoto wao. Dalili hizo kwa kawaida huendelea hatua kwa hatua, lakini baadhi ya watoto wenye ugonjwa wa akili hukua kwa kawaida kijumla kabla ya ukuaji kubadilika. Ingawa mwingilio wa mapema wa kitabia au wa kitambuzi unaweza kuwasaidia watoto wenye ugonjwa wa akili kujihimili, kupata ujuzi wa kijamii, na mawasiliano, hakuna tiba inayojulikana. Si watoto wengi wenye usonji huishi kwa kujitegemea wanapofikia utu uzima, ingawa baadhi huwa wafanisi. Kumeibuka desturi ya usonji, huku watu wengine wakitafuta matibabu na wengine wakiamini lazima usonji ikubalike kuwa utofauti, si ugonjwa.


© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search